Kubeti kwa kutumia akili au kistaarabu ni njia ya kujitambua na kubashiru bila maumivu makubwa, watu wengi hubashiri kama wamelewa bila kitumia akili na kujikuta wanaishi katika majuto makubwa, katika makala haya nitakueleza mbinu mbimbali za kubeti kwa kutumia akili.
Beti bila kuzingatia Ushabiki Hii ni njia ya kubeti kwa kuzingatia uwezo wa timu husika, uwezo wa wachezaji, ugumu wa mchezo , bila kujali timu unayoibetia unaipenda ama laa, mara nyingi wengi hubashiri kwa kuzingatia ushabiki au jina la timu husika na kujikuta wakipoteza bila sababu ya msingi.
Fanya utafiti Kabla ya kubeti, Ndio , utafiti ni muhimu, angalia msimamo, angalia Head to Head, angalia vikosi, angalia mbinu za makocha, angalia uwiano wa kufunga na kufungwa, angalia hali ya majeruhi ya vikosi, angalia mwenendo wa timu nzima, taarifa hizi zinaweza kukupa mwanga
Tambua Kubeti ni starehe na sio Kazi au chanzo Cha mapato , Michezo ya kubashiri inatakiwa kuchukuliwa kama starehe na sio kama chanzo kikuu cha mapato, kama hauna kazi ni muhimu kutafuta kazi ya kufanya,, kuifanya betting kuwa chanzo cha mapato siku utakayokosa au kupoteza fedha unaweza kuanguka katika msongo mkubwa wa mawazo. Nimuhimu kuwa na chanzo cha mapato na betting ibaki kama starehe tu isiyo starehesha.
Beti kiwango unachoweza kumudu , Kubeti kiwango unachoweza kumudu ikiwa utapoteza ni jambo la muhimu sana, beti kulingana na uwezo wako na sio kushawishiwa na watu walioweka madau makubwa, hakikisha umepangilia bajeti yako na unaweka kiwango ambacho hata ukipoteza hutapata maumuvu. Nimuhimu kuweka bajeti na kamwe usivuke bajeti hiyo
Jua wakati sahihi wa kupumzika au Kuacha, HilI ni jambo la muhimu sana wakati wa kubashiri au kucheza casino mtandaoni, nimuhimu sana kujua wakati wakuacha kucheza , kupumzika au kujiondoa kabisa, kucheza kwa hasira au kuendelea kucheza utaendelea kupokea vipigo mfululizo jambo ambalo linaweza kuathiri moja kwa moja uchumi na akili yako.
Kuepuka Kucheza kwa lengo la kurudisha Hasara kwa pupa
Kwa kawaida michezo ya kubashiri huambatana na kupata na kukosa , huku kupoteza kukiwa na nafasi kubwa zaidi , inapotokea umepoteza fedha acha kutaka kuirudisha kwa pupa au hasira, kyfanya hivyo kunaweza kukusababisha kupoteza zaidi.
Fahamu Hakuna Fixed games au Usinunue Mkeka, Hili ni jambo la muhimu sana , epuka matapeli wanaojifanya kukuzia matokeo mtandaoni, kufanya hivyo kunaweza kukufanya upoteze mara mbili. Fahamu hakuna anayeweza kujua matokeo kabla ya mchezo na kuwa kushinda nibahati. Jiulize kama anayekuuzia anajua ticket hiyo itashinda kwanini asiiwekee fedha nyingi ili ashinde yeye? Watu wa familia yake? Nimuhimu kuzingatia jambo hili.
Mwisho:
Betting ni mchezo unaombatana na kuweza kujidhibiti mwenyewe, ukiona unakuathiri ni muhimu kuacha kuliko kuendelea, kama umekuwa addicted unaweza kuwasiliana na bodi ya michezo ya bahati nasibu kwa msaada zaidi.

Post a Comment